1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauji ya mbunge yahatarisha mdahalo ya kitafa nchini Lebanon

Charo, Josephat11 Septemba 2008

Kiongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu Amr Mussa aalikwa kufungua mkutano kuhusu mdahalo wa kitaifa

Mauaji ya mbunge wa Lebanon kunahatarisha juhudi za kuleta maridhiano ya kitaifa ambazo tayari zimekwamishwa na mipasuko ya makundi yanayohasimiana nchini humo. Rais wa Lebanon, Michel Suleiman amemualika kiongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu Amr Mussa kuhudhuria mkutano wa kitaifa utakaoanza Jumanne wiki ijayo.

Viongozi wa Lebano hii lo wametoa mwito kuwepo utulivu nchini kote huku mauaji ya kwanza ya kisiasa yakitishia juhudi za kiyaunganisha makundi yaliyogawanyika. Sheikh Saleh Aridi, mbunge wa chama cha Lebanese Democratic aliuwawa katikashambuliola bomu jana jioni katika mji wa Baysur, kusini mashariki mwa mji mkuu Beirut, kwenye makazi yake.

Afisa wa usalama amesema bomu lililotengenezwa kutumia gramu 700 ya vifaa vya kulipuka lilitegwa chiniy motokaa yake. Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo.

Marekani imelilaani vikali shambulio hilo ambalo liliwajeruhi kidogo watu wengine sita. Msemaji wa wizara ya mamboy andaniy a Marekani, Sean McCormack, amesema katika taarifa yake kwamba Marekani haitayumbishwa katika kuiunga mkono serikali ya Lebanon na tasisi zake za kidemokrasia.

Rais wa Lebanon, Michel Suleiman ameonya dhidi ya juhudi zozote kuvuruga juhudi za kutafuta maridhiano ya kitaifa zinazoendelea, huku mauaji hayo ya kwanza ya mbunge anayeegemea Syria, yakiwa yamefanyika siku moja baada ya rais Suleiman kutangaza kuanza kwa mdahalo wa vyama mbalimbali nchini Lebanon Jumanne ijayo. ´´Lazima tujihadhari na njama zinazolenga kufuja juhudi za kuleta maridhiano na matayarisho ya mdahalo wa kitaifa,´´ amesema rais Michel Suleiman.

Rais Suleiman amemualika kiongozi ya jumuiya ya nchi za kiarabu Amr Mussa kuhudhuria mkutano wa kitaifa kuhusu mdahalo na maridhiano ulioapngwa kuanza Jumanne wiki ijayo katika ikulu ya Baabda. Mussa amealikwa kuufungua mkutano huo kwa mujibu wa makubaliano ya Doha yaliyofikiwa kati ya wanasiasa wa Lebano mwezi Mei mwaka huu.

Sheikh Saleh Aridi, akiwa katika umri wa miaka ya 50 alikuwa mshauri mkuu wa kiongozi anayeiunga mkono Syria na ambaye ni waziri wa Lebanon, Talal Arslan, hasimu wa kiongozi wa madhehebu ya Druze, Walid Jumblatt anaipinga Syria. Jumblatt amelilaani shambulio dhidi ya mbunge huyo na kulieleza kuwa juhudi ya kuchochoea machafuko kati ya chama chake na chama cha Arslan, ambavyo vilifikia mapatano mnamo mwezi Mei mwaka huu baada ya mapambano makali kati ya makabila yanayohasimiana.

Mbunge wa Druze Marwan Hamadeh amesema kuuwawa kwa Aridi kumefanywa na watu wanaotaka mdahalo wa kitaifa usifaulu.

Sheikh Saleh Aridi ambaye chama chake kinashirikiana na kundi la wanamgambo wa kishia la Hezbollah, ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu anayeiunga mkono Syria kuuwawa tangu mfululizo wa mashambulio ya mabomu yalipoanza nchini Lebanon mnamo mwaka wa 2005, yakiwalenga hasa wanasiasa wanaoipinga Syria.

Wakati Lebanon ikikabiliana na shambulio la jana, raia wanne wa Syria na Mlebanon mmoja wameuwawa wakati lori lililokuwa limesheheni fashifashi za magendo kutoka Syria lilipolipuka hii leo mashariki mwa Lebanon karibu na mpaka kati ya Lebanon na Syria.