1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMauritania

Mauritania na Mali zatafuta suluhu mvutano wa mpakani

21 Aprili 2024

Waziri wa Ulinzi wa Mauritania aliwasili nchini Mali jana kwa mazungumzo na kiongozi wa kijeshi, huku nchi hzo jirani zikitarajia kuusuluhisha mgogoro kuhusu machafuko ya mpakani.

Kiongozi wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goita |
Kiongozi wa mpito wa Mali Kanali Assimi GoitaPicha: Alexander Ryumin/TASS Host Photo Agency via REUTERS

Karibu wiki mbili kabla, Mauritania ililituhumu Kundi la Mamluki wa Urusi la Wagner kwa kuwasaka watu waliokuwa na silaha hadi ndani ya mpaka wa Mauritania. Kufuatia tukio hilo, Bamako iliutuma ujumbe wa ngazi ya juu mjini Nouakchott kujaribu kutuliza mivutano.

Hapo Jana, kiongozi wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goita, alimpokea Waziri wa Ulinzi Hanena Ould Sidi. Wakati wa mazungumzo yao, Waziri Sidi alisifu kile alichokiita uhusiano wa kidugu na kihistoria kati ya nchi hizo jirani, na kusisitiza haja ya kudumisha na kuimarisha uhusiano wao.

Ijumaa, Mauritania ilimuita balozi wa Mali kulalamikia mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya raia wasio na hatia na wasioweza kujilinda.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Mauritania ilisema katika taarifa kuwa hali hiyo isiyokubalika imekuwa ikiendelea licha ya onyo lililotolowa na nchi hiyo.