1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauwaji yaendelea Congo licha ya sheria ya kijeshi

Saleh Mwanamilongo
10 Juni 2021

Wanajeshi zaidi wa Umoja wa Mataifa kupelekwa Kivu na Ituri, huku mauwaji ya raia yaki ongezeka maradufu. Jeshi la Congo pia latangaza hatua zaidi.

Kongo | Flüchtlinge in Ituri
Picha: imago-images/Xinhua/A. Uyakani

Msemaji wa jeshi la Congo, FARDC, jenerali Richard Kasongo amewambia wandishi habari mjini Kinshasa kuwa jeshi limezidisha operesheni zake dhidi ya makundi yote ya wapiganaji na ndio sababu waasi hao wamelipiza kisasi kuwashambulia raia.

'' Tumeendesha operesheni kabambe ambayo lengo lake ni kuyasambaratisha makundi ya wapiganaji likiwemo lile la ADF huko Beni. Bila shaka operesheni hizo zilizaa matunda kwa sababu ngome zote za waasi hao zilidhibitiwa na jeshi.'',alisema Kasonga.

 Kauli hiyo ya msemaji wa jeshi imekuja siku 30 baada ya Rais Tshikedi kutangaza sheria ya kijeshi kwenye mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Ituri.

Hospitali ya chomwa moto na waasi

Shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka MSF lilieleza kuwa waasi walichoma moto hospitali ya Boga ambako shirika hilo lilikuwa likiwahudumia raia.

Kwenye barua yao ya wazi kwa Waziri Mkuu wabunge wa Kivu ya Kaskaini na Ituri wamesema kuwa mnamo kipindi cha wiki moja zaidi ya raia 57 wameuliwa kwenye mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Ituri.

Umoja wa Mataifa umesema utawapeleka wanajeshi wake zaidi huko Beni na Ituri ilikuwalinda raia. Hatua hiyo hata hivyo haijachangia kukomesha mashambulizi ya waasi hao, amesema Kizito bin hangi kiongozi wa msharika ya kutetea haki za binadamu kwenye mtaa wa Beni.

''Ni toka siku nyingi wanajeshi wa Monusco wanasema watapigana na waasi wa ADF ,lakini kwa nini ADF inaendelea kuuwa raia na Umoja wa mataifa haufanye chochote?'', alijohi Bin Hangi. '' Kwa kweli huo ujumbe wa wanajeshi wa Monusco hautusaidii'',aliendelea kusema.

Raia waendelea kukimbia makazi yao

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa laorodhesha wakimbizi wapya jimboni Ituri.Picha: picture-alliance/dpa/H. Wasswa

Mapema wiki hii,Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limesema mashambulizi hayo ya kundi la ADF yamesababisha watu wapatao 5,800 kukimbia katika kambi kadhaa kwenye jimbo la Ituri.

Shirika hilo limetaka usalama uimarishwe katika eneo hilo ili kuwalinda raia, wengi ambao wamelazimika kuyakimbia makazi yao mara kadhaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW