Mauzo ya magari ya umeme yaliongezeka 2024 kwa asilimia 25
14 Januari 2025Hayo ni kulingana na takwimu zilizochapishwa leo na kampuni ya teknolojia ya Uingereza inayokusanya data juu ya mauzo ya magari, Rho Motion.
Magari ya umeme milioni 17.1, bila ya kujumuisha magari ya mseto yanayotumia mafuta na wakati huo huo umeme, yaliuzwa duniani kote mwaka jana.
China imeendelea kuongoza na kuwa soko kubwa zaidi la magari ya umeme duniani, nchi hiyo ikiuza magari ya umeme milioni 11, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Soma pia: Je, EU inaanzisha vita vya biashara na China
Barani Ulaya, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Iceland, Norway na Uswizi, mauzo ya magari ya umeme yalishuka kwa asilimia tatu hadi magari milioni 3 baada ya miaka minne ya ukuaji mkubwa.
Mauzo ya magari ya umeme pia yaliongezeka nchini Marekani na Canada, yakipanda kwa asilimia tisa hadi magari milioni 1.8.