Mavazi ya kila aina yahanikiza Carnival inapoanza Ujerumani
11 Novemba 2025
Mji wa Cologne umeanza msimu wa sherehe za Carnival siku ya Jumanne, huku malefu ya watu wakikusanyika kwenye mji huo ambao ni kitovu cha sherehe hizo.
Maelfu ya watu wakisherehekea mwanzo wa msimu wa karnivali huko Heumarkt, Cologne Novemba 11, 2025Picha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance
Matangazo
Msimu wa Carnival huanza rasmi tarehe 11.11 majira ya saa tano za asubuhi. Na siku ya Jumanne, mapema kabisa wahudhuriaji wa mwanzo waliokuwa wamevalia mavazi ambayo mengi hustaajabisha tayari walikuwa wamekusanyika kwenye mji wa Cologne ulioko katika Jimbo la North Rhine Westphalia, magharibi mwa Ujerumani.
Ilipofika majira ya saa mbili za asubuhi, tayari kulikuwa na mistari mirefu mbele ya baadhi ya bar na maeneo ya kujivinjari. Na kama mshereheshaji mmoja wa runinga Guido Cantz alivoywahi kusema "Sio kila kitu kinawezekana mjini Cologne lakini, tunajua namna ya kujivinjari."
Usalama waimarishwa
Zaidi ya maafisa wa polisi 1,000 na wengine 450 wa kulinda usalama wa umma na walinzi wa makampuni binafsi 1,200 wako macho kuhakikisha usalama wa wahudhuriaji kwenye sherehe hiyo ya Carnival, ambako huwa kunafurika watu katika msimu huo.
Afisa wa polisi akiwapiga picha wahudhuriaji wa sherehe za kanivali waliovalia mavazi ya "kifahari" mwanzoni mwa msimu wa kanivali mjini ColognePicha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance
Lakini huenda wakazuia watu kuwa na visu wakati wa sherehe na kuwarai watu kujizuia kuvaa ama kuwa na vitu vinavyoweza kutumika kama silaha.
Kama ilivyokuwa mwaka uliopita, sinagogi kubwa kabisa mjini Cologne lililoko karibu na mtaa wa wanafunzi pia utalindwa kwa namna ya kipekee kabisa.
Kanivali duniani kote: Kutoka Rio hadi Rhine
Kinachoitwa na Wajerumani ‘msimu wa sita’ kinakaribia kumalizika: sherehe za wiki ya mwisho kabla ya Kwaresima, ambapo watu wanatoa mavazi yao na kushereheka – na sio tu Ujerumani bali duniani kote.
Picha: Reuters
Rio de Janeiro, Brazil
Mavazi ya kuonyesha miili, ming'aro na samba - hayo ndiyo mambo yanayoshamiri katika kanivali hiyo maarufu duniani kote. Watu wapato 90,000 kwa siku sita mfululizo mjira ya jioni, huwa wanayasindikiza magwaride ya shule za ngoma ya samba. Baadae, sherehe zinaendelea barabarani, katika baa na migahawa.
Picha: picture-alliance/dpa/Citypress24
Venice, Italy
Hili ni tamasha maarufu kwa watu kuvaa nyuso zenye mapambo ya aina yake, ambalo lilianzishwa 1286. Watu wanazificha nyuso zao na kusherehekea bila ya kujulikana utambulisho wao.
Picha: Getty Images/AFP/A. Pizzoli
Oruro, Bolivia
Wanaokwenda katika kanivali hii lazima wasiwe na woga wa kina, kwa vile mji mkuu wa mkoa wa Oruro upo mita 3700 juu ya usawa wa bahari. Nyuso zilizotengenezwa kwa mikono na mavazi ya kijadi ndiyo vitu vinavyopewa umuhimu katika sherehe hizi ambazo hufanyika barabarani, kwa siku tatu. Ni sherehe zinazoashiria pande mbili za mwanadamu; ubaya na wema.
Picha: picture-alliance/robertharding/C. Kober
New Orleans, USA
Mardi Gras, ni siku ya kwanza ya Kwaresima, ambayo inasherehekewa katika mji wa New Orleans nchini Marekani. Kawaida kunakuwa na gwaride za watu waliovalia mavazi tofauti pamoja na muziki wa jazz, hasa katika eneo hili lenye historia na asili ya Kifaransa.
Picha: picture-alliance/dpa/D. Anderson
Quebec, Canada
Lakini je ukiambiwa uende kwenye kanivali wakati hali ya hewa ni nyuzi joto -30? Hapo lazima upate kinywaji cha Caribou, ambacho ni mchanganyiko wa pombe ya brady, vodka, sherry na mvinyo. Sherehe hizo huwa na mtu anayetengenezwa kwa theluji aliepewa jina la Bonhomme Carnaval, mashindano ya ridha na magwaride makubwa ya muziki huku baridi na theluji vikiwa vimetawala.
Picha: picture-alliance/empics/J. Boissinot
Mohács, Hungary
Kanivali za Ulaya Mashariki mara nyingi asili yake ni hadithi za jadi, kama ilivyo katika mji wa kusini mwa Hungary wa Mohács. Kwa karne kadhaa imekuwa ni desturi yao kutoka kwenye baridi wakiwa wamejifunika nyuso zilotengenezwa kwa ubao, na mavazi ya ngozi ya kondoo. Tamasha la Busó mjini Mohács limekuwa katika orodha ya UNESCO kama turathi ya dunia tokea 2009.
Picha: picture-alliance/dpa/MTI/T. Soki
Mainz, Germany
Katika Weiberfastnacht, “Siku ya Kanivali ya Wanawake,” wanawake huwa wanazikata tai za wanaume na kuwapa mabusu. Kanivali hiyo inayosherehekewa barabarani huwa na mavazi ya rangi nyingi na furaha nyingi hutandaa. Sherehe zinakuwa na muelekeo wa kisiasa zaidi Jumatatu ya mawaridi. Nchini Ujerumani hasa karibu na miji ya mto Rhine, sherehe zote zinamalizika Jumatano ya Majivu.
Picha: picture alliance/dpa/A. Arnold
Bonoua, Ivory Coast
Je kuna kanivali Afrika? Bila shaka! Kila mwaka Aprili mamia kwa maelfu ya watu wanautembelea mji wa Bonoua kusini mwa Ivory Coast, kusherehekea tamasha la Popo (nyuso).
Picha: picture-alliance/dpa/L. Koula
Picha 81 | 8
huanza tarehe 11.11 kila mwaka, ikiwa ni siku ya 11 ya mwezi wa 11. Cologne huwa ni kitovu cha sherehe hizo, lakini miji mingine ya karibu kama Dusseldorf na Bonn pia hufurika watu kuadhimisha.
Sherehe hizo humalizika siku ya Jumatano ya Majivu, ambayo huangukia Februari 18, ikiwa ndio siku ya kwanza ya kuanza msimu wa Kwaresma kwa Wakristo ulimwenguni.