1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri kadhaa bado wapo kazini Syria

9 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Syria amesema mawaziri kadhaa bado wanafanya kazi mjini Damascus hata baada ya waasi kuuteka mji mkuu na kumpindua Rais Bashar al Assad.

Syrien | Ende des Assad Regimes - Feier in Damaskus
Picha: Bekir Kasim/Anadolu/picture alliance

Waziri Mkuu Mohammed Ghazi Jalali, ambaye amebakia katika wadhifa wake baada ya Assad na maafisa wake kadhaa wakuu kutoweka, anafanya bidii ya kuonesha kuwa hali ni ya kawaida.

Amesema anafanya kazi ili kipindi cha mpito kikamilishwe kwa haraka na kwa urahisi. Waziri mkuu huyo ameeleza kuwa hali ya usalama imeboreka.

Pia amesema serikali inawasiliana na waasi na kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa waasi hao, Abu Mohammed al-Golani.

Misururu ya wakimbizi walivuka kutoka nchi jirani na kuingia Syria wakiwa na matumaini ya mustakabali wa amani zaidi.

Hata hivyo tayari pana dalili za matatizo mnamo siku sijazo kuhusu umoja wa waasi wanaodhibiti sehemu kubwa ya nchi, wanaoongozwa na Abu Mohammed al -Golani aliyekuwa mpiganaji wa kundi la kigaidi la al- Qaeda ambaye baadaye alijitenga na kundi hilo ameahidi kuleta serikali wakilishi na stahamala ya kidini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW