1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri Uingereza wafadhaishwa na mchakato wa Brexit

Isaac Gamba
2 Oktoba 2017

Mawaziri waandamizi katika serikali ya waziri mkuu wa Uingereza Theresa May wanaonekana kufadhaishwa kutokana na kwenda taratibu kwa mazungumzo ya mchakato wa Brexit.

Florenz, britische Premierministerin Theresa May hält Rede
Picha: Reuters/A.Tarantino

Katika mkutano wa chama tawala cha wahafidhina- Conservative uliofanyika mjini Manchester kaskazini mwa London Waziri wa fedha wa Uingereza Philip Hammond  alififisha umuhimu wa masharti mapya yanayopaswa kufuatwa katika mazungumzo hayo ya Brexit yaliyotolewa na waziri wa mambo ya nje ya nchi hiyo  Boris Johnson ambayo yanaonekana kuleta mgawanyiko katika baraza la mawaziri la serikali ya waziri mkuu Theresa May.

Philip Hammond aliieleza televisheni ya Uingereza  ya ITV kuwa wote wamechanganyikiwa kufuatia kwenda taratibu kwa mazungumzo yanayohusina na Uingereza kuijiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na kuwa ndiyo sababu Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alikwenda Florence siku kumi zlizopita na kutoa hotuba ambayo ilikuwa inalenga kuondoa vikwazo vinavyochelewesha mazungumzo hayo na kuchukua hatua mathubuti za kuwezesha mazungumzo hayo kweda kama inavyopasa.

Waziri huyo wa fedha wa Uingereza alisema msimamo wa waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson katika suala hilo unafahamika  na kusisitiza  kuwa anakubaliana na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kufuatia  kususua kwa mazungumzo ya Brexit  na nia yake ya kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo yanafanyika kwa kuzingatia jinsi walivyo elekezwa na wananchi wa Uingereza kwa ajili ya masilahi ya taifa hilo. 

Matamshi ya Hammond yanakuja mnamo wakati waziri huyo akitarajiwa kutoa hotuba kwenye  mkutano wa kila mwaka wa chama cha Conservative ambao unachukuliwa kama mwanya wa serikali ya Waziri Mkuu Theresa May kujaribu kurejesha imani kati ya serikali na wafuasi wa chama hicho kufuatia matokeo mabaya ambayo chama hicho kilipata wakati wa uchaguzi wa mapema mwezi Juni.

 

Chama cha Labour chanufaika na kufanya vibaya kwa  Conservative

Kiongozi wa chama cha Labour Jeremy CorbynPicha: picture alliance/PA Wire/D. Lipinski

Matokeo hayo yalikifanya chama cha Consevative kupoteza imani kwa wapiga kura hatua ambayo ilioneonekana kukinufaisha chama cha Labour kinachoongozwa na msoshalisti Jerome Corbiny.

Katika kuelekea  mkutano huo  Philip Hamond  ambaye alishika wadhifa wa uwaziri wa fedha kuanzia Julai 2016 alizungumzia pia juu ya umuhimu wa soko huria kiuchumi na kuwa ndiyo njia pekee katika kusitawi kiuchumi.

Amesema siyo bahati mbaya kuwa kila nchi  ulimwenguni ukiacha Korea Kaskazini, Venezuela, Zimbabwe na Cuba  zinafuata mfumo wa soko huria unaofuatwa pia na Ungereza na kuongeza kuwa hilo limetokea kwa sababu inafahamika vema kuwa  hiyo ndiyo njia pekee kwa mataifa mbalimbali kustawi kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha ya watu wake pamoja na kutengeneza nafasi za kazi.

Hata hivyo mawazo hayo yanayoneka kupingwa na  Chama cha upinzani cha Labour  ambacho katika mkutano wake mkuu  wiki iliyopita kiligusia juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali ya Conservative ikiwa ni pamoja na matumizi ya gharama kubwa katika serikali pamoja na utozaji mkubwa wa  kodi.

Mwandishi: Isaac Gamba/rtre

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW