1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Armenia na Azerbaijan kukutana Washington

10 Julai 2024

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Azerbaijan na Armernia wanakutana leo mjini Washington kwa duru mpya ya mazungumzo yanayodhamiria kutafuta mkataba wa amani baina ya mataifa hayo mawili hasimu.

Trilaterales Treffen Deutschland, Armenien und Aserbaidschan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Azerbaijan, Jeyhun Bayramov, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Armenia, Ararat Mirzoyan Berlin, Februari 28, 2024.Picha: Thomas Trutschel/photothek/IMAGO

Tangazo la mkutano huo limetolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Armenia na kuthibitishwa na ofisi ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.

Nchi hizo mbili jirani zimepigana vita mara mbili kuwania jimbo lililojitenga la Azerbaijan la Nagorno Karabakh ambalo lilikuwa na wakaazi wengi wenye asili ya Armenia. Mwaka jana Azerbaijanilichukua udhibiti wa jimbo katika operesheni yake ya siku moja na kuwalazimisha zaidi ya Armenia 100,000 kulikimbia.

Juhudi za upatanishi za miaka mingi  zimeshindwa kumaliza mivutano ya nchi hizo  lakini viongozi wake wameashiria miezi ya hivi karibuni kwamba mkataba wa amani uko mbioni kupatikana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW