UchumiUlaya
Mawaziri wa biashara wa Ulaya wakosoa ushuru wa Trump
15 Julai 2025
Matangazo
Mawaziri hao waliokutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, wamesema tangazo la Trump la kutaka kuweka kiwango hicho cha ushuru "halikubaliki" na wameapa kuwa watachukua hatua za kujibu mapigo.
Mkutano wao umefanyika baada ya Trump kuelezea azma yake ya kuzitoza ushuru bidhaa kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya, uamuzi unaotishia kuwa na taathira kwa serikali, kampuni na walaji wa pande zote mbili.
Trump alisema ushuru huo mpya utaanza kufanya kazi Agosti mosi kama hakutapatikana makubaliano baina ya pande hizo mbili.
Mawaziri hao wa biashara wamesema watafanya kazi pamoja kutafuta kataba wa biashara na Marekani au watachukua hatua za kujibu mapigo.