Mawaziri EU wahadhari wito wa kususia mikutano ya Hungary
22 Julai 2024Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels, kujadili kuhusu mgogoro wa Ukraine na Mashariki ya Kati, wamezungumzia kwa tahadhari pendekezo la kuususia mkutano ujao usiokuwa rasmi ulioandaliwa kufanyika mjini Budapest, Hungary.
Pendekezo hilo limetolewa kufuatia ghadhabu zilizoenea,Umoja wa Ulaya dhidi ya waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban kutokana na hatua aliyoichukuwa hivi karibuni ya kufanya ziara kivyake, mjini Moscow katika kile alichokiita ujumbe wa amani.
Soma pia:Mawaziri wa EU kukutana na kuijadili Ukraine na Gaza
Orban alimtembelea pia rais Xi Jinping mjini Beijing na mgombea urais wa Marekani wa chama cha Republican, Donald Trump.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Annalena Baerbockwakati akiwasili kwenye mkutano wa leo mjini Brussels amesema, ziara za siku chache za kiburi zilizofanywa na Orban zimesababisha hasira lakini mwenye maamuzi ya kutoa agizo la kuusisia mkutano wa Hungary ni Joseph Borrell ambaye ni mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya.