1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU wakutana kujadili usaidizi kwa Ukraine

1 Desemba 2025

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amesema wiki hii itakuwa na umuhimu kwa ajili ya juhudi za kumaliza vita vya Ukraine.

Ubelgiji Brussel 2025 | Kaja Kallas akizungumza na waandishi wa habari
Kaja Kallas asema wiki hii ni muhimu kwa masuala ya kidiplomasia yanayolenga kumaliza vita vya Urusi nchini UkrainePicha: Dursun Aydemir/Anadolu/picture alliance

Wawakilishi wa Marekani wanaelekea Moscow baada ya mazungumzo na wapatanishi wa Kiev.

Akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amesema hii inaweza kuwa wiki muhimu kwa masuala ya kidiplomasia. Amesema wamesikia kuwa mazungumzo yaliyofanyika Marekani yalikuwa magumu lakini yenye tija.

Kulingana na Kallas, hawajui bado matokeo yake, lakini baadae Jumatatu atazungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi wa Ukraine.

Steve Witkoff, mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump, Jumatatu ataelekea Urusi, wakati ambapo Marekani inashinikiza kuvimaliza vita vya Urusi dhidi ya jirani yake Ukraine.

Aidha, Kallas amesema umoja huo ulikuwa umeazimia kufikia makubaliano ya ufadhili wa Ukraine katika mkutano wa kilele wa viongozi utakaofanyika Desemba 18, akisema hawatamaliza bila kufikia makubaliano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW