Mawaziri wa EU wahimiza mshikamano mbele ya utawala wa Trump
21 Januari 2025Matangazo
Mawaziri hao wamekubaliana kwamba uchumi imara katika Umoja wa Ulaya utakaotowa ushindani ni silaha bora ya kupambana na changamoto kutoka Marekani.
Katika kikao chao kisichokuwa rasmi cha chakula cha usiku,mawaziri wa fedha wa mataifa 27 ya Umoja huo wa Ulaya pia walikubaliana, kwamba mahusiano thabiti na Marekani ni muhimu kwa maslahi ya pande zote mbili Umoja huo wa Ulaya na Marekani.
Trump asaini maagizo kadhaa ya rais
Kadhalika, wengi wa mawaziri hao waliunga mkono kwamba hatua ya kujumuisha masoko zaidi ya nishati itakuwa na manufaa makubwa kwa jumuiya hiyo.