1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiCanada

Mawaziri wa Fedha wa G7 waahidi kuleta usawa wa kiuchumi

23 Mei 2025

Mawaziri wa Fedha na magavana wa Benki Kuu wa Kundi la G7 waliwekapembeni tofauti zao jana Alhamisi na kuahidi kushughulikia suala la ukosefu wa usawa katika uchumi wa dunia.

Canada Banff | Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa G7
Mawaziri wa Fedha na magavana wa Benki Kuu wa kundi la G7 wakiwa kwenye mkutano wa kundi hilo nchini CanadaPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Mawaziri hao wa G7 aidha wamekubaliana juu ya uwezekano wa kuongeza vikwazo dhidi ya Urusi.

Waziri wa Fedha wa Canada Francois-Philippe Champagne aliwaambia waandishi wa habari kwamba waliafikiana kwa pamoja juu ya maswala muhimu zaidi ya kiulimwengu yanayowakabili.

Kabla ya mkutano huo kulikuwa na shaka ikiwa kungetolewa taarifa ya pamoja kwa kuzingatia migawanyiko kuelekea ushuru wa Marekani na vita vya Urusi nchini Ukraine.

Mkutano huu unafungua milango ya mkutano wa kilele wa wakuu wa G7, Juni 15-17 katika eneo la mapumziko la mlima la Kananaskis, nchini Canada, ambapo Rais Donald Trump atahudhuria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW