1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Mawaziri wa G7 kujadili mzozo wa Gaza na Ukraine

25 Novemba 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la mataifa saba tajiri duniani G7 wanakutana karibu na mji wa Rome mazungumzo ya siku mbili na wenzao wa kanda ya Mashariki ya kati kuhusu vita vya nchini Ukraine.

Mawaziri wa Kundi la G7 wakiwa kwenye mkutano wao nchini Italia
Mawaziri wa Kundi la G7 wakiwa kwenye mkutano wao nchini Italia. Picha: Andreas Solaro/AFP via Getty Images

Mawaziri hao wa G7 watajadili pia juu ya waranti wa kukamatwa iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkuu wa kijeshi wa kundi la Hamas, na athari zinazoweza kujitokeza katika vita vya sasa vya Gaza na Lebanon.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atahudhuria mazungumzo hayo pamoja na mawaziri wengine wa Uingereza, Canada, Ujerumani, Ufaransa, Japan na mwenyeji wao Antonio Tajani wa Italy.

Leo Jumatatu, mkutano huo utajikita katika mzozo wa mashariki ya kati na Bahari ya Sham, hasa juhudi za kufikia usitishaji wa mapigano ukanda wa Gaza na Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW