SiasaJapan
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa G7 kujadili usalama wa Ulaya
14 Aprili 2023Matangazo
Mkutano huo wa siku tatu utakaoanza mnamo Jumapili kwenye mji wa mapumziko wa Karuizawa unafanyika chini ya kiwingu cha vita kati Urusi na Ukraine na kuongezeka kwa kitisho cha China dhidi ya kisiwa cha Taiwan.
Soma pia: Wanadiplomasia wa G7 washikamana na Ukraine
Afisa mmoja wa wizara ýa mambo ya nchi za nje ya Japan amesema usalama wa Ulaya na kanda ya bahari ya Hindi na Pasifiki hauwezi kujadiliwa kwenye jukwaa tofauti kwa sababu yanafungamana.
Mkutano huo utakaowaleta pamoja mawaziri kutoka Marekani, Japan, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Canada na Italia ni maandalizi ya mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa nchi za G7 utakafanyika Hkwenye mji wa Hiroshima mwezi ujao.