1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa kigeni wa G7 wakutana juu ya Ukraine

11 Novemba 2025

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa G7 wanakutana nchini Kanada kwenye mikutano inayotazamiwa kujikita kwenye mzozo wa Ukraine na Urusi na kusaka njia ya pamoja ya kukomesha vita hivyo.

Kanada Kananaskis 2025 | G7
Viongozi wa mataifa ya G7 walipokutana mwezi Juni nchini Kanada.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Mkutano huo unaofanyika kwenye mkoa wa Nagara unaopakana na Marekani unatarajiwa kuzungumzia  ufadhili zaidi kwa Ukraine.

Mawaziri hao wanakutana baada ya Rais Donald Trump kuziwekea vikwazo kampuni mbili kubwa kabisa za mafuta za Urusi mwezi uliopita, na kumkosoa vikali Rais Vladimir Putin kwa kukataa kukomesha vita hivyo.

Trump pia ameyashinikiza mataifa ya Ulaya kuacha kununuwa mafuta ya Urusi, akidai kuwa fedha wanazotowa ndizo zinazotumiwa na Moscow kuendeleza vita vyake nchini Ukraine.

Licha ya Kiev kuendelea kukabiliwa vibaya na mashambulizi ya Moscow, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kanada, Anita Anand, amejizuwia kuahidi hatua zotote madhubuti kuisaidia Ukraine kwenye mazungumzo hayo ya Niagara.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW