1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa kigeni wa Ulaya kukutana leo

20 Machi 2023

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels, huku ajenda kuu zikiwa kununua risasi za Ukraine, vikwazo vipya vya Iran na yanayoendelea Tunisia.

Belgien | Treffen EU-Außenminister | Runder Tisch
Picha: European Union

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba anatarajiwa kuwafahamisha mawaziri wenzake kwa njia ya video kuhusu hali ilivyo sasa.

Mawaziri wa Ulinzi wa  Umoja wa Ulaya watashiriki katika mjadala kuhusu mipango ya kuipatia Ukraine dola bilioni 2, kwa ajili ya kupeleka haraka makombora Ukraine.

Wanadiplomasia hao wanatarajiwa kuweka vikwazo vipya kwa Iran kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali. Hatua kadhaa zilizochukuliwa na Rais wa Tunisia Kais Saied, ili kuimarisha mamlaka yake pia ni ajenda itakayojadiliwa leo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW