1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa NATO wakutana Brussels kujadili usalama

3 Desemba 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO, wanakutana mjini Brussels kuzungumzia usalama na vita vya Ukraine.

Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Picha: TANG CHHIN SOTHY/via REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atashiriki mkutano huo ambao huenda ukawa wa mwisho wa ngazi za juu kushiriki, kabla utawala wa rais Joe Biden kuondoka madarakani. 

Miongoni mwa ajenda za mwanzo kwenye mkutano huo ni suala la kuimarisha uungaji  mkono kwa Ukraine kabla ya kurudi Donald Trump madarakani Januari mwakani. 

Rais Zelensky aitaka Marekani iushawishi Umoja wa Ulaya ukubali kuikaribisha Ukraine NATO

Masuala ya kipaumbele katika ushirikiano wa kiusalama kati ya Marekani na Ulaya yatajadiliwa ikiwemo kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi, lakini pia kuimarisha ushirikiano na washirika wa NATO wa kusini katika kanda ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, na Sahel. Mkutano huo pia utajadili maandalizi ya mkutano ujao wa kilele utakaofanyika The Hague mwezi Juni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW