Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Afrika wakutana Kampala
23 Julai 2010Matangazo
Nchini Uganda,kikao cha mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Afrika kimeendelea leo katika mji mkuu wa Kampala, kabla ya Viongozi wakuu wa nchi hizo kuanza kukutana hapo kesho. Mapema alasiri ya leo Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Jean Ping alikua na mkutano na waandishi habari ambapo miongoni mwa mengine akatangaza kwamba Guinea na Djibouti ziko tayari kutuma wanajeshi nchini Somalia. Mwandishi wetu mjini Kampala Leylah Ndinda alikuwako mkutanoni na hii hapa ripoti kamili.
Mtayarishaji; Leylah Ndinda
Mpitiaji:Thelma Mwadzaya.