1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wajiandaa kuijadili Sudan

22 Mei 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa hii leo kuijadili hali ya nchini Sudan baada ya Saudi Arabia na Marekani kusimamia makubaliano ya kusitishwa vita kwa siku saba kati ya pande mbili zinazozozana.

Schweden | informelles Treffen der EU-Außenminister in Stockholm
Picha: Jonas Ekstromer/TT News Agency/REUTERS

Siku ya Jumapili, mashambulizi ya anga,ufyetulianaji risasi uliendelea kushuhudiwa katika mji mkuu Khartoum kabla ya kutangazwa makubaliano hayo.

Usitishaji mapigano unatarajiwa kutowa nafasi ya kupelekwa msaada wa kibinadamu kwa raia nchini humo na unatarajiwa kuanza baadae leo Jumatatu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Marekani na Saudi Arabia,Jumamosi Jioni kufuatia mazungumzo yaliyofanyika Jeddah.

Soma pia: Nchi zenyeushawishi zatakiwa kusuluhisha mzozo wa Sudan

Nchi hizo mbili kwenye taarifa yao ya pamoja zilikiri juu ya kukiukwa kwa makubaliano ya awali lakini zikasema makubaliano ya safari hii ni tofauti. Umoja wa Afrika,Umoja wa Mataifa na jumuiya ya ushirikiano wa kiserikali wa nchi za mashariki mwa Afrika IGAD zimeyapongeza makubaliano hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW