1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mawaziri wa mambo ya nje wa G20 wakutana India

1 Machi 2023

Mzozo wa Urusi na Ukraine unatarajiwa kuchukua sehemu muhimu ya mazungumzo katika mkutano wa kilele wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 20 zilizostawi kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi huko nchini India.

Indien | Treffen der Finanzminister und Notenbankchefs der G20
Picha: Aijaz Rahi/AP Photo/picture alliance

Mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa India Vinay Kwatra anasema wana imani kwamba changamoto za kiuchumi zilizotokana na vita hivyo zitaangaziwa kwa usawa pia.

Soma pia:Mkutano wa G20 wamalizika bila makubaliano muhimu kuhusu vita vya Urusi na Ukraine

Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe 40 wakiwemo mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mwenzake wa Marekani Antony Blinken na Qin Gang wa China. Mazungumzo yatafanyika hapo kesho baada ya chakula cha jioni leo.

Kundi la G20 linajumuisha nchi saba tajiri zinazojumuisha muungano wa G7 pamoja na Urusi, China, India, Brazil, Australia na Saudi Arabia miongoni mwa nchi zengine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW