1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Saudi waahidi kuumaliza mzozo wa Sudan

15 Julai 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan, wameonyesha dhamira yao ya kuumaliza mzozo nchini Sudan na kupeleka misaada ya kibinadamu.

Faisal Bin Farhan Al Saud na Antony Blinken
Faisal Bin Farhan Al Saud na Antony BlinkenPicha: Jonathan Ernst/AP Photo/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Marekaniimesema kuwa wawili hao walizungumza jana kwa njia ya simu.

Mapigano yaliyozuka Aprili 15 yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao katika maeneo ya mji mkuu Khartoum, Bahri na Omdurman na kuchochea vita vya kikabila katika jimbo la Darfur.

Juhudi za upatanishi za kikanda na kimataifa hadi sasa zimeshindwa kuutatua mzozo huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW