1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRomania

Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO kukutana

29 Novemba 2022

Katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens Stoltenberg anatarajiwa kuwatolea mwito washirika wa jumuiya hiyo kutoa ahadi ya msaada zaidi kwa Ukraine, katika kipindi hiki cha majira ya baridi kali.

Rumänien Nato-Generalsekretär Jens Stoltenberg zu Besuch in Bukarest
Picha: ANDREI PUNGOVSCHI/AFP

Wito huo unatarajiwa kutolewa katika mkutano utakaofanyika leo na kesho Jumatano. Kadhalika wito huo unakuja baada ya rais wa Ukraine kuwaambia wananchi wake kutarajia wiki nyingine ya baridi na kiza kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na Urusi dhidi ya miundo mbinu ya Ukraine.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya NATO watakaokutana mjini Bucharest, nchini Romania watajikita kuzungumzia hatua ya kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga pamoja na silaha pamoja na msaada usiokuwa wa kijeshi kama mafuta, vifaa tiba, na vifaa vinavyotumika wakati wa baridi kali.

Ujerumani ambayo hivi sasa  inashikilia uongozi wa kundi la nchi tajiri kiviwanda duniani,G7  nayo inapanga mkutano na baadhi ya washirika wa kundi hilo pembezoni mwa mkutano huo wa NATO wakati ikijaribu kushinikiza hatua za kuharakisha ujenzi mpya wa miundo mbinu ya nishati ya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW