SiasaUhispania
Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya kuijadili Niger
31 Agosti 2023Matangazo
Mawaziri hao wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia wameeleza kufuatilia juu ya kinachoendelea Gabon baada ya jeshi kutangaza kutwaa madaraka.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amewaambia waandishi wa habari kuwa, mapinduzi nchini Niger yamefungua enzi mpya ya kukosekana kwa utulivu katika ukanda wa Sahel ambao tayari unakumbwa na uasi.
Kukosekana kwa utulivu katika nchi za Afrika Magharibi na Kati, na vita vya nchini Ukraine ni baadhi ya ajenda watakazozijadili kwenye mkutano wao mjini Toledo.
Hassoumi Massoudou, waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Niger iliyoondolewa madarakani na Omar Touray, mkuu wa tume ya ECOWAS pia watahudhuria mkutano huo.