1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wakutana Brussels

16 Desemba 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels kujadili hali ya sasa nchini Syria pamoja na Georgia, Ukraine,mashariki ya kati na hali ya kisiasa nchini Belarus.

Belgien Brüssel 2024 | Treffen der EU Innenminister | Nancy Faeser und Leon Gloden
Picha: Omar Havana/AP Photo/picture alliance

Kikao hicho ambacho kitaongozwa kwa mara ya kwanza na mkuu mpya wa sera za nje wa Umoja huo wa Ulaya, Katja Kallas, pia kinajiandaa kuidhinisha duru ya 15 ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi tangu nchi hiyo ilipovamia Ukraine Februari 2022.

Waziri wa mambo ya nje wa ukraine Andrii Sybiha nae pia anatarajiwa kushiriki mkutano huo kwa njia ya video kutowa sura ya hali ilivyo kwa sasa katika uwanja wa vita.

Kadhalika mkutano huo unafanyika wakati suala la uwezekano wa Umoja wa Ulaya kuhusika katika kupeleka kikosi cha kulinda amani, likipata nguvu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW