1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mawaziri wa nje wa ASEAN bado hawajakubaliana juu ya Myanmar

13 Julai 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kusini Mashariki ya Asia (ASEAN) bado wanatafuta njia ya kupata msimamo wa pamoja kuhusu mgogoro wa Myanmar.

Indonesien ASEAN Gipfel
Picha: Achmad Ibrahim/AP Photo/picture alliance

Mawaziri hao wanakutana kwenye mji mkuu wa Indonesia, Jakarta, kuujadili mgogoro huo pamoja na usalama wa eneo lao.

Licha ya mwenyekiti wa mkutano, Indonesia, kutoa wito wa kuleta suluhisho la kisiasa nchini Myanmar, lakini mawaziri wa ASEAN bado hawajakubaliana juu ya tamko la pamoja.

Soma zaidi: Indonesia yahimiza suluhisho la kisiasa Myanmar
Waziri wa mambo ya nje wa Thailand akutana na Suu Kyi

Hata hivyo, mwanadiplomasia mmoja amesema mawaziri hao wanaendelea na bidii ya kufikia mwafaka na huenda taarifa ya pamoja ikatolewa baadaye.

Hakuna maelezo yaliyotolewa juu ya kuchelewa taarifa hiyo ya pamoja kwa muda mrefu.

Waziri wa mambo ya nje wa Indonesia amesema wajumbe wa nchi hiyo wamekutana na wajumbe wa pande zote za mgogoro wa nchini Mynmar katika juhudi za kuleta suluhisho.