1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mawaziri wa Uingereza na Ujerumani ziarani Israel

17 Aprili 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Cameron na wa Ujerumani Annalena Baerbock wam,ekutana na Rais wa Israel mjini Jerusalem na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana dhidi ya Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David cameron (kulia), rais wa Israel Isaac Hergoz (katikati) na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena baerbock mjini Jerusalem
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David cameron (kulia), rais wa Israel Isaac Hergoz (katikati) na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena baerbock mjini Jerusalem Picha: Ilia Yefimovich/dpa/picture alliance

Annalena Baerbock ameutolewa wito Umoja wa Ulaya kuiwekea Iran vikwazo vipya vitakavyoilenga teknolojia yake ya droni huku Cameron akisema ni wazi kuwa Israel imechukua uamuzi wa kujibu mashambulizi ya Iran lakini akasema anatumai kuwa hilo litaendeshwa kwa kuzingatia hatari ya kutotanuka kwa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati.

Hayo yakiarifiwa, Rais wa Iran ameonya leo kuwa uvamizi wowote japo mdogo wa Israel utajibiwa vikali, katika wakati ambapo kuna uwezekano wa Israel kulipiza kisasi  baada ya shambulio kubwa la Iran siku ya Jumamosi. Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo katika gwaride la kila mwaka la jeshi ambalo mara hii lilifanyika katika kambi ya kaskazini mwa mji mkuu, Tehran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW