Mawaziri wa Ujerumani na China kukutana leo
28 Juni 2011Matangazo
Mawaziri hao wa China wamo katika ujumbe wa Waziri mkuu wa nchi hiyo, Wen Jiabao, ambaye yuko Ujerumani kwa ziara ya siku mbili.
Aliwasili jana jioni na kupokewa na Kansela Angela Merkel.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle alisema kwamba atagusia suala la haki za binadamu nchini humo wakati wa ziara hiyo ya Waziri mkuu wa China, hapa nchini.