1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Ukraine wajiuzulu kufuatia sakata la ufisadi

13 Novemba 2025

Mawaziri wa sheria na nishati nchini Ukraine, German Galushchenko na Svitlana Hrynchuk, wamejiuzulu jana Jumatano kufuatia madai ya kuhusika kwao na sakata kubwa la ufisadi katika sekta ya nishati nchini humo.

Ukraine Kiev 2025 | Waziri wa sheria German Galushchenko
German Galushchenko, mshirika mkuu wa Rais wa Ukraine anadaiwa kuanzisha mpango wa ufisadi wa dola milioni 100 katika sekta ya nishati Ukraine.Picha: Danylo Antoniuk/Ukrinform/IMAGO

Wachunguzi wamedai kuwa Galushchenko, mshirika mkuu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alianzisha mpango wa ufisadi wa dola milioni 100 katika sekta hiyo, hali iliyosababisha hasira ya wananchi wakati ambao taifa linakosa umeme kufuatia mashambulizi ya Urusi yanayoendelea kushamiri huko.

Ukraine imekuwa ikikabiliwa na kashfa mbalimbali za ufisadi, na kuondoa tatizo hilo serikalini ni moja ya masharti yanayohitajika ili kujiunga na Umoja wa Ulaya. 

Awali Rais Zelensky aliwataka mawaziri hao kujiuzulu kufuatia uchunguzi wa sakata ya hilo ufisadi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW