1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Ulaya kujadili uungaji mkono kwa Ukraine

12 Desemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock anapanga kufanya mazungumzo leo na mawaziri wenzake kadhaa, pamoja na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas, kuhusu kuiunga mkono zaidi Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock.Picha: Mauersberger/IMAGO

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imeeleza kuwa mkutano huo unakusudia kupeleka ujumbe wa wazi wa kuendelea kuiunga mkono Ukraine kwa kuzingatia mabadiliko yajayo ya rais nchini Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Berlin.

Mbali na kujadiliana kuhusu msaada wa kijeshi, kifedha na kiutu kwa Ukraine, wanadiplomasia hao pia watazungumzia hali ya maendeleo nchini Syria, na athari zake katika ukanda huo.

Mbali na Kallas na Sybiha, Baerbock amewakaribisha pia mawaziri wenzake kutoka Ufaransa, Poland, Italia, Uhispania na Uingereza.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW