Mawaziri wa ulinzi mataifa matano kujadili usalama wa Ulaya
25 Novemba 2024Matangazo
Hatua ya Urusi ya kuishambulia Ukraine kwa makombora mapya ya kuvuka mabara, ambayo inatajwa kuwa na athari kwa bara zima la Ulaya, huenda ikawa ajenda kuu ya majadiliano hayo.
Mkutano huo unafanyika pia kabla ya kuapishwa rasmi mnamo Januari 20 Rais mteule wa Marekani Donald Trump ambaye ni mkosoaji mkubwa wa jumuiya ya kujihami ya NATO.
Kiongozi huyo wa Marekani ameitaka Ulaya kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika usalama wake wenyewe na huenda pia akapunguza kiwango cha msaada wa kijeshi kwa Ukraine.