1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani, Urusi wajadili kupunguza hatari za kusambaa mzozo

13 Julai 2024

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amezungumza kwa simu na Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Angrei Belousov, hii ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Singapore | Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekano Lloyd Austin akutana na mwenzake wa Urusu kujadili vitisho dhidi ya usalama wa ulimwenguPicha: Vincent Thian/AP/dpa/picture alliance

Wizara za ulinzi za nchi hizo zimearifu kwamba kwenye mazungumzo hayo ambayo Pentagon imethibitisha yaliratibiwa na Moscow, Austin na Belousov walijadiliana juu ya kupunguza hatari ya kile walichosema "uwezekano wa kusambaa" kwa mvutano katikati ya ongezeko la wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili, baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Mazungumzo hayo, yanafanyika siku mbili tu baada ya Marekani kutangaza itapeleka makombora ya masafa marefu nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.

Mjini Washington, Naibu msemaji wa Pentagon Sabrina Singh aliwaambia waandishi wa habari kwamba "waziri alisisitiza umuhimu wa kudumisha njia za mawasiliano katikati ya vita vinavyoendelea vya Urusi dhidi ya Ukraine."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW