Mawaziri wa Ulinzi wa Urusi, Iran na Syria wakutana Moscow
24 Aprili 2023Matangazo
Hayo yametangazwa leo na waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar.
Akar amesema lengo la mazungumzo hayo yatakayofanyika Moscow kesho Jumanne, ni kusuluhisha matatizo ambayo yamesababishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria na kupatikana kwa amani ya kanda hiyo.
Nchi zote zinazohudhuria mkutano huo zilihusika katika vita vya Syria, huku Urusi na Iran zikiunga mkono utawala wa rais Bashar al-Assad na Uturuki ikiwaunga mkono waasi kutoka kaskazini mwa Syria.
Mnamo mwezi Disemba, mawaziri wa ulinzi wa Syria, Urusi na Uturuki walikutana mwanzo ili kutuliza mvutano kati ya Damascus na Ankara.