Mawaziri wakubaliana kuyasimamisha mapigano mashariki mwa Ukraine
3 Julai 2014Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank - Walter Steinmeier amesema ili kuutatua mgogoro wa Ukraine lazima mapigano yasimamishwe.
Mawaziri wa Ujerumani,Ufaransa, Urusi,Ukrainea na Poland wamekubaliana juu ya kuchukua hatua kadhaa ili kuweza kuyasimamisha mapigano mashariki mwa Ukraine. Hatua hizo ni pamoja na kuyaanzisha mazungumzo haraka ili kulifikia lengo la kuyasimamisha mapigano katika msingi wa muda mrefu, bila ya masharti, na kukubalika na pande zote .Mawaziri hao pia wamekubaliana kwamba hatua ya kuyasimamisha mapigano isimamiwe na Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya,OSCE
Wakati huo huo ,majeshi ya serikali ya Ukraine yameimarisha mashambulio dhidi ya wapiganaji wanaoegemea upande wa Urusi ambao wanaotaka kujitenga. Msemaji wa Bunge la Ukraine ameeleza kwamba majeshi ya usalama yanaendelea kuwashambulia wapinzani wa mashariki mwa nchi hiyo kwa kushrikiana na vikosi maalumu.
Rais wa Ukraine apinga kusimamisha mapigano
Rais Petro Poroshenko amelipinga pendekezo la kuurefesha muda wa kuyasimamisha mapigano na ameyaamuru majeshi ya nchi yake yaendelee kuyajibu mashambulio ya waasi wa mashariki mwa Ukraine.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir ameonya dhidi ya kurejea katika hali ya kuukoleza zaidi mgogoro wa Ukraine. Waziri Steinmeier amesema mambo yanaweza kuripuka nchini humo na kufikia kiwango cha kushindikana kudhibitiwa tena kisiasa au kijeshi.
Mazungumzo kufanyika kupitia majopo ya mawasiliano
Mawaziri wa mambo ya nje wa,Urusi, Ukraine,Poland, Ufaransa na mwenyeji wao waziri Steinmeier wa Ujerumani wametamka wazi kwamba mazungumzo juu ya kusimamisha vita nchini Ukraine yatafanyika kwa njia ya majopo ya mawasiliano
Hali ya wasi wasi imetanda baada ya Rais Poroshenko wa Ukraine kukataa kuurefusha muda wa kuyasimamisha mapigano dhidi ya waasi wa mwashariki mwa Ukraine. Kwa mujibu wa taarifa mapambano ni makali katika miji ya jimbo la Donetsk. Majeshi ya Ukraine yamefanya mashambilio kwa kutumia ndege.
Majeshi ya Ukraine yatafanikiwa?
Juu ya juhudi za majeshi ya serikali ya Ukraine kiongozi wa wabunge wa chama cha kijani katika bunge la Ulaya Rebecca Harms amesema hawezi kutathmini hata kidogo iwapo mashambulio ya majeshi ya serikali ya Ukraine yatafanikiwa lakini amesema kila serikali inataka kuilinda ardhi yake"
Mwandishi:Mtullya Abdu rtre,afpe,
Mhariri:Yusuf Saumu