1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

May aahidi kufanikisha Brexit

Sekione Kitojo
4 Oktoba 2017

Theresa May ameomba radhi kwa chama chake kwa matokeo ya uchaguzi uliokwenda kombo na kuahidi msaada wa kiuchumi kwa familia zenye mapato hafifu, huku akijaribu kurejesha msukumo katika serikali yake iliyogawika.

Großbritannien Manchester Parteitag Konservative Theresa May
Picha: Imago/i Images/A. Davlin

Amedokeza  pia kwamba  anataka mazungumzo  ya  kujitoa  kutoka  Umoja wa  Ulaya , Brexit  yafanikiwe.

Katika  hotuba  aliyoitoa  katika  mkutano  mkuu  wa chama  ambayo  ilijaa  lugha  ya kinadharia na  kuingiliwa kati  na  mtu wa  kufanya masihara, May  amesema kampeni  ya  uchaguzi  ilikuwa "kama  imeandikwa, na iliyoelekea  katika  hali  ya  urais zaidi."

"Niliongoza  kampeni , na  nawataka  radhi ,"  amesema.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa MayPicha: Reuters/P. Noble

Wahafidhina  wamekasirika  baada  ya  uchaguzi  wa mapema  wa  mwezi  Juni  ulioitishwa  miaka  mitatu  kabla kwa  matumaini  ya  kuimarisha  wingi  katika  chama chake  bungeni, lakini  uchaguzi  huo  ulishuhudia  serikali ya  May  ikipungukiwa  wingi.

Matokeo  hayo  mabaya  yamemdhoofisha  May  na anahangaika  kuleta  umoja  katika  serikali  yake kuhusiana  na  masuala  ya  Brexit  na  kadhalika.

May  amesema.

"Chama  cha  kihafidhina  kinapaswa  kuahidi  kurejesha ndoto ya  Waingereza  katika  nchi  hii  kwa  mara  nyingine tena."

Mazungumzo ya  Brexit

Serikali  ya  Uingereza  inataka  majadiliano  ya  Brexit yafanikiwe  lakini  inajitayarisha  pia  na  hali  ambayo yanaweza  kushindwa, waziri  mkuu  Theresa  May amewaambia  wanachama  wa  chama  chake  cha Conservative  katika  mkutano  wa  mwaka  leo.

Waandamanaji wanaopinga Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa UlayaPicha: Reuters/M.Rossi

"Naamini  ni kwa  maslahi  kila  mmoja  wetu  kwa  majadiliano  hayo kufanikiwa  lakini  nafahami  kwamba  baadhi wana  wasi wasi  iwapo  tuko  tayari  itakapotokea  kwamba yatashindwa. Ni  wajibu  wetu  kama  serikali  kujitayarisha kwa  hilo," May  amesema.

"Wakati  wapinzani  wetu  wanakumbatia  sera  za mambo ya  kigeni za  kati  kwa  kati  na  kujitayarisha  kupambana. Baadhi  ya  watu  wanasema  tumetumia  muda  mrefu kuzungumzia maisha ya zamani  ya  Jeremy Corbyn. Kazi yetu  ya  kwanza  muhimu  sana  ni  kufanikisha  Brexit. watu  wameamua, tumechukua maelekezo  yao. Uingereza inajitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya Machi 2019."

May  amefunga  mkutano  huo  wa  mwaka  wa  chama chake  kwa  hotuba akiwaambia  mawaziri  wake  kujiweka na  kulenga  katika  maisha  ya  kawaida  ya  wafanyakazi. katika  juhudi  za  kuwavutia  wapiga  kura  wenye  kipato cha  chini  na  kati , May  ameahidi  kuweka  ukomo  wa  bei na malipo kwa  ajili  ya  nishati  na kuifanya  serikali irejea katika  shughuli  za  ujenzi wa  nyumba kwa  ajili  ya wananchi.

Theresa May akiingia katika ukumbi wa mkutano mkuu wa chama cha ConservativePicha: Reuters/H. McKay

Alikuwa  akizungumza , siku  moja  baada  ya  bunge  la Umoja  wa  Ulaya  kwa  kauli  moja  kuunga  mkono  hoja inayoyotoa  wito  wa  mazungumzo  ya  kibiashara na Uingereza  kucheleweshwa kwasababu  mazungumzo hayajapiga  hatua ya  kutosha.

Bunge  la  ulaya  mjini  Strasbourg  limeishambulia serikali ya  May , likisema  mivutano  ya  ndani  katika  baraza  lake la  mawaziri  inazuwia  mazungumzo na masuala  muhimu ya  kutengana  ikiwa  ni  pamoja  na  fedha  zinazopaswa kulipwa  na  Uingereza  kwa ajili ya  kujitoa.

Mwandishi :  Sekione Kitojo / afpe / ape

Mhariri: Idd Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW