1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

May aahidi kushinda mapambano ya fikra

Admin.WagnerD11 Julai 2017

Akijaribu kupata kasi ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kumuacha akiwa dhaifu Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema inabidi ashinde mapambano ya fikra bungeni na katika nchi.

UK | Theresa May
Picha: picture alliance/AP Photo/M. Dunham

Katika hotuba ambayo ilikuwa na mambo yote mawili ya upatanishi na ukaidi May amewahamiza wapinzani wake wa kisiasa kuchangia mawazo yao na fikra ili kusaidia kujenga sera wakati wa kipindi cha mabadiliko makubwa ya taifa wakati Uingereza ikijitowa Umoja wa Ulaya.

May amesema kujitolea kwake kuibadili Uingereza hakukufifia ikiwa takriban mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani na kama mwezi mmoja tu baada ya kubebeduliwa na wapiga kura katika uchaguzi aliouitisha kwa haraka.

Amekaririwa akisema :"Nasema kwa vyama vyengine katika bunge isomeni repoti hii jishughulisheni na matatizo magumu inayoyazusha.Jitokezeni na mwazo na fikra zenu vipi tunaweza kukabiliana na changamoto hizi kama nchi. Tunaweza tusikubaline kila kitu lakini kwa kupitia midahalo na majadiliano alama zetu za demokrasia bungeni,fikra zinaweza kuainishwa na kuboreshwa na njia nzuri ya kuosonga mbele ikapatikana na huo ndio mwamko utakaoipeleka mbele agenda hii miezi inayokuja."

Kamari ya kisiasa yamuangusha

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.Picha: Getty Images/WPA Pool/M. Dunham

May alikuwa waziri mkuu wa Uingereza hapo tarehe 13 mwezi wa July mwaka 2016 kufuatia ushindani wa kuwania uongozi wa chama chake cha Conservative baada mtangulizi wake aliyekuwa waziri mkuu  David Cameron kujiuzulu wakati wapiga kura walipoamuwa kinyume na usahuri wake kujitowa Umoja wa Ulaya May aliitisha uchaguzi na mapema katika juhudi za kuimarisha mamlaka yake wakati wa mazungumzo ya kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

Kamari hiyo ya uchaguzi aliyoicheza imemgeuka wakati wapiga kura walipokinyima chama cha Conservative wingi wao wa viti bungeni na kukiongezea viti bungeni chama cha mrengo wa kati kushoto cha Labour.

Matokeo hayo yamemaanisha May lazima ategemee kufikia makubaliano na muafaka kupitisha miswada ya sheria bungeni na kiko mbioni kukishawishi chama cha Ireland Kakazini cha DUP kukiunga mkono.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AP

Mhariri: Yusuf Saumu