1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

May awataka wapiga kura kuunga mkono mpango wake wa Brexit

Sekione Kitojo
16 Novemba 2018

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alikuwa akitapia kunusuru wadhifa wake leo baada ya makubaliano ya mswada wa talaka na  Umoja wa Ulaya kuzusha kujiuzulu kwa mawaziri waandamizi na miito ya kura ya kutokuwa na imani.

Großbritannien Proteste in London | pro-Brexit
Picha: Reuters/H. Nicholls

Zaidi  ya  miaka  miwili  baada  ya  Uingereza kupiga  kura kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya , bado  haijafahamika  ni vipi, katika  masharti  gani  ama  hata  iwapo  nchi  hiyo itaweza  kujitoa  kutoka  Umoja  huo kama  ilivyopangwa yaani  Machi 29, mwaka  2019.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May Picha: Reuters/T. Melville

May ambaye  aliingia  katika  wadhifa  huo  wa  juu kutokana  na  mtafaruku  uliofuatia  kura  ya  maoni  ya mwaka  2016, imeamua  kufanya  majadiliano  kuhusu makubaliano  ya  Brexit  ili  kuhakikisha taifa  hilo  linajitoa kwa  njia  bora  zaidi. Waziri  wa  fedha  wa  Ufaransa Bruno Le Maire  amesema  kila  nchi  ina  haki  ya  kujitoa kutoka  Umoja  huo. 

"Tunaweza  kufanya, bila  shaka. Kila  nchi iko  huru kuamua  kujitoa  kutoka  katika  soko  hili  la  pamoja, kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya. Lakini kile  Brexit inachoonesha  ni  kwamba gharama  za  kiuchumi  za kujitoa  katika  soko  la  pamoja  ni kubwa  mno. Na kwamba  kwa kweli  wanadanganya  na  wanasiasa wasiowajibika nchini  Uingereza  ambao  wanawaambia watu  wa  Uingereza  kwamba  Brexit  itaishia katika  hali bora  ya  hapo  baadaye."

Waandamanaji wakipinga kujitoa Uingereza katika Umoja wa UlayaPicha: Reuters/K. Coombs

Sarafu ya Pauni yaporomoka

Nae  waziri wa  Brexit  Dominic Raab  alijiuzulu  jana kuhusiana  na  makubaliano  hayo, na  kusababisha  sarafu ya  pouni  kuporomoka. Wabunge  waasi  katika  chama chake  waliamua  wazi  kupinga  uongozi  wake  na kumwambia  wazi  kwamba  makubaliano  ya  Brexit hayatapita  bungeni.

May, ambaye  ameapa  kubakia  kuwa  waziri  mkuu, aliombwa  na  mwananchi  mmoja  aliyepiga  simu  katika redio LBC " kujiuzulu  kwa  heshima". Hakuweza  mara moja  kulijibu  swali  hilo  la msikilizaji  huyo. Waziri  mkuu May  aliwatolea  wito moja  kwa  moja  wapiga  kura kuunga  mkono mpango  wake  wa  Brexit huku  akipata changamoto  kubwa  kwa  uongozi  wake  kutoka mahasimu  wake  katika  chama  chake.

"Kwa watu  wengi  waliopiga  kura  ya  kujitoa," kile walichotaka  kufanya  ni  kuhakikisha  kwamba  uamuzi kuhusu  masuala  kama  nani  anaingia  katika  nchi  hiyo yatafanywa  na  sisi  nchini  Uingereza, na  sio mjini Brussels, na  hicho  ndio  hasa makubaliano  niliyofikia yanachotoa,"  alisema  May.

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark RuttePicha: Reuters/V. Kessler

Waziri mkuu  wa  Uholanzi Mark Rutte amesema  leo kuwa Umoja  wa  Ulaya hautakuwa  radhi  kubadili makubaliano yanayopendekezwa ya  Brexit iwapo yatatupiliwa  mbali  na bunge  la  Uingereza.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / ape

Mhariri: Mohammed  Abdul-Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW