1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

May na Kenyatta kushirikiana zaidi

30 Agosti 2018

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amezuru Kenya na kusaini mikataba kadhaa na Rais Kenyatta, ukiwemo wa kuimarisha vita dhidi ya ufisadi. Uingereza itaisaidia Kenya kurejesha mali za mafisadi zilizoko nchini humo.

Theresa May na Uhuru Kenyatta
Picha: DW/S. Wasilwa

M M T/ J3 30.08.2018 Theresa May in Kenia - MP3-Stereo

This browser does not support the audio element.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amewasili nchini Kenya hivi leo na kutiliana saini mikataba kadhaa na taifa hilo la Afrika Mashariki, ukiwemo ule wa kuimarisha vita dhidi ya ufisadi. Kwenye mkataba huo Uingereza itaisaidia Kenya kurejesha mali za mafisadi zilizoko nchini humo. Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa serikali yake haitalegeza kamba dhidi ya ufisadi ili kufikia malengo yake. Kwa upande wake, waziri mkuu wa Uingereza ametoa hakikisho kuwa nchi yake itashirikiana na Kenya kuafikia lengo hilo. Mwanahabari wetu Shisia Wasilwa alihudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika ikulu ya Nairobi na kutuandalia ripoti ifuatayo.