Maziwa kutoka China marufuku nchini Burundi na Tanzania
23 Septemba 2008Matangazo
Kwa sasa mkaguzi mkuu wa usalama wa chakula nchini humo tayari amefutwa kazi kufuatia taarifa hizo.Jumla ya watoto wanne wanaripotiwa kufariki jambo lililopelekea baadhi ya mataifa kupiga marufuku uingizaji na usambaaji wa maziwa na bidhaa za maziwa kutoka Uchina.Mataifa hayo yanajumuisha Bangladesh,Brunei,Japan,Malaysia,Myanmar,Singapore,Burundi na Tanzania.Kemikali ya melamine hutumika kutengezea bidhaa za plastiki na husababisha athari za figo katika mwili wa binadamu.
Ili kupata ufafanuzi wa hatua hiyo nchini Tanzania Thelma Mwadzaya amezungumza na Gaudencia Simwaza afisa wa uhusiano katika Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa.