1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo baina ya Marekani na Urusi kuhusu silaha nzito

Saleh Mwanamilongo
28 Julai 2021

Maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani na Urusi wamekutana mjini Geneva kwa mazungumzo kuhusu udhibiti wa silaha za nyuklia.Mkutano huo umefuatia ule wa Biden na Putin mwezi Juni.

Russland Interkontinentalrakete
Picha: picture-alliance/AP Photo/RU-RTR

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Wendy Sherman na mwenziye  Sergei Ryabkov wa Urusi wameongoza jumbe wa nchi zao kwenye mazungumzo hayo ya mjini Geneva. Duru zinaelezea kwamba mazungumzo baina ya pande hizo mbili yamefanyika kwenye ubalozi wa Marekani nchini Uswisi.

 Rais wa Marekani Joe Biden na Vladimir Putin wa Urusi,ambao nchi zao zinamiliki asilimia 90 za jumla ya silaya ya nuklia ulimwenguni,walikubaliana mwezi Juni, kuendesha mazungumzo ya kimkakati ili kuweka misingi ya kudhibiti silaha katika siku za usoni.

 Ajenda rasmi ya mazungumzo hayo ya siku moja haikufahamika,lakini wataalamu wamehisi ni mwanzo wa mchakato huo baina ya nchi hizo mbili.

Daniel Hogsta wa shirika la kimataifa la kupambana na silaha za nuklia,ameliambia shirika la Reuters kwamba mazungumzo hayo ni lazima yazingatiye umuhimu wa kupunguza silaha za nuklia.

Tofauti zisizo kwisha baina ya Marekani na Urusi

Marekani na Urusi zilirefusha muda wa mkataba wa kudhibiti matumizi ya silaha za kimkakati za nyuklia kwa miaka mitano

Andrey Baklitskiy, mtafiti mkuu kwenye kituo cha utafiti kuhusu Marekani ,mjini Moscow amewambia waandishi habari mjini Geneva kuwa mkutano huo unatarajia kuweko na baadhi ya maelewano baina ya pande mbili, mwaka mmoja baada ya mkutano wa aina hiyo kufanyika.

Mwezi Januari, Urusi ilikubaliana na Marekani,kurefushwa kwa muda mkataba wa kudhibiti umiliki wa silaha za nyuklia kati ya Marekani na Urusi uitwao New START kwa miaka mitano. Mkataba unazilazimu Marekani au Urusi kutotumia zaidi ya vichwa vya nyuklia 1,550 vya kimkakati.Pande mbili hizo zimetarajiwa kujadili aina ya silaha zinazo zusha wasiwasi kubwa baina yao.

Urusi yamkosoa Biden 

Huku hayo ya kijiri, Urusi imesema leo kwamba kimsingi rais wa Marekani Joe Biden amekosea na tathmini yake kuhusu nchi hiyo. Matamshi hayo yamefuatia kauli ya Rais Biden hiyo jana kwamba uchumi wa urusi ni dhaifu, hali ambayo ina iweka nchi hiyo katika hali ngumu kiuchumi.

Biden aliituhumu pia urusi kujaribu kuingilia kati uchaguzi mdogo wa bunge wa Marekani wa mwaka 2022 na kuwa rais Putin ameongoza nchi ambayo inategemea tu silaha za kinyuklia na visima vya mafuta.

 Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin amesema matamshi hayo sio sahihi. Peskov amesema Urusi inanguvu ya kinyuklia,lakini nguvu hiyo imetumiwa ipasavyo na Urusi inamiliki pia sekta kubwa ya mafuta na gesi. Lakini kusema Urusi haika kitu kingine mbali na hivyo kimsingi ni sio kweli.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW