SiasaEthiopia
Mazungumzo kati ya serikali na waasi wa OLA yaanza Tanzania
26 Aprili 2023Matangazo
Msemaji wa kundi hilo la OLA Odaa Tarbii ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mazungumzo yanafanyika visiwani Zanzibar.
Msemaji huyo ameeleza kwamba mazungumzo haya yanalenga kuanzisha msingi wa majadiliano ya kina katika siku za usoni na kuongeza kuwa Kenya na Norway ni wapatanishi.
Ameserma hatua ya sasa ya mazungumzo hayo inahusisha kujenga uaminifu kati ya pande mbili na kufafanua nafasi zilizopo.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza wiki iliyopita kwamba mazungumzo na kundi la waasi la OLA yataanza siku ya Jumanne.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Stergomena Tax aliwaambia waandishi wa habari kwamba Tanzania imekubali ombi la kuandaa mazungumzo hayo.