SiasaColombia
Colombia: Serikali yaanza mazungumzo ya amani na waasi
9 Oktoba 2023Matangazo
Kulingana na Tume ya Juu ya Colombia, wapatanishi kutoka serikalini na wajumbe wa kundi la Estado Mayor Central (EMC) wanakutana kuanzia siku ya Jumapili katika manispaa ya Tibú karibu na mpaka wa Venezuela kwa ajili ya mazungumzo hayo ya amani.
Wajumbe wa pembeni kwenye mazungumzo hayo ni Umoja wa Mataifa Marekani, Kanisa Katoliki, Umoja wa Ulaya, Norway, Uswizi, Ireland na Venezuela.
Soma pia:Colombia yaongoza kwa mauaji ya wanaharakati wa mazingira
Rais wa Colombia Gustavo Petro amesema mazungumzo ya amani na kundi la waasi la mrengo wa kushoto la ELN pia yanaendelea na pia ameyaalika makundi mengine ya waasi na wanamgambo kushiriki kwenye katika mazungumzo hayo ya amani.