1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Amani ya Ukraine yaahirishwa hadi Jumatano

1 Februari 2026

Duru ya pili ya mazungumzo kati ya maafisa wa Urusi, Ukraine na Marekani kuhusu mpango wa Marekani wa kumaliza vita vya Ukraine sasa imepangwa kuanza Jumatano, badala ya Jumapili.

Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye hata hivyo hakutoa sababu ya kucheleweshwa kwa mazungumzo hayo.

Tangazo hili linajiri siku moja baada ya mjumbe wa ngazi ya juu wa Rais Vladimir Putin kufanya mazungumzo ya kushtukiza na maafisa wa Marekani huko Florida bila ya uwepo wa Ukraine.

Mazungumzo hayo ya pande tatu yanatarajiwa kufanyika Abu Dhabi tarehe 4 na 5 Februari, ingawa Marekani na Kremlin bado hawajathibitisha rasmi tarehe hizo.

Washington inasisitiza kuwa iko karibu kufikia makubaliano ya kumaliza vita ambavyo vimekuwa vya umwagaji damu zaidi barani Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Hata hivyo, suala la mipaka bado limekwama, huku Urusi ikitaka udhibiti kamili wa jimbo la Ukraine la Donbas, lakini Ukraine inapinga vikali mkataba wowote wa kuilazimisha iachie ardhi yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW