Mazungumzo ya amani Yemen njia panda
7 Septemba 2018Shirika la habari la Saudia Arabia Al Arabiya limesema kuwa upande wa serikali umeweka muda wa mwisho kuwa jumamosi kwa waasi wa Houthi ambao bado hawajaondoka kutoka mji mkuu wa yemen Sanaa kuwa wamewasili Geneva au utajiondoa kutoka kwenye meza ya mazungumzo.
‘Hatutawasubiri waasi wa Houthi milele mjini Geneva' amesema waziri wa mambo ya kigeni wa Yemen Khaled Alyemany anayeongoza ujumbe wa serikali lakini bila kuanisha tarehe ya ukomo na wao kuondoka.
Umoja wa Mataifa hata hivyo umesema kupitia msemaji wake kuwa hauna taarifa juu ya ukomo wa kusubiri uliotolewa na upande wa serikali ya Yemen.
Serikali ya Yemen ilitoa taarifa siku ya ijumaa ikiwalaumu waasi wa Houthi na kuongeza kuwa kutoonekana kwa ujumbe wa kundi hilo kumedhiirisha lengo lao la kurudisha nyuma hatua za umoja wa mataifa kuelekea amani ya kudumu na kumaliza mateso kwa watu wa yemen.
Mazungumzo hayo ambayo yangekuwa ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili baina ya pande hasimu nchini yemen yalipangwa kufanyika siku ya alhamisi mjini Geneva.
Wahouthi wanataka usafiri salama
Hadi mapema ijumaa Waasi wa Houthi walio na mafungamano na Iran walikuwa bado hawajaondoka kutoka mji mkuu wa Yemen; Sana'a baada ya kukataa kuabiri ndege ya Umoja wa Mataifa kwa madai kuwa hawakupewa hakikisho la kurejea Yemen baada ya mazungumzo.
Waasi hao wanasisitiza kusafiri kwenda Geneva kwa kutumia ndege kutoka taifa jirani la Oman wakisema ihatahakihisha kurejea kwao salama nchini Yemen.
Siku ya alhamisi kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi hilo la waasi Mohammed Ali al-Houthi alisema kupitia Twitter kuwa muunngano unaongozwa na Saudia Arabia na unaouunga mkono serikali inayotambuliwa kimataifa ulikataa kutoa ruhusa kwa ndege ya Oman kuusafirisha ujumbe wake kenda Geneva.
Kulingana na kiongozi huyo, hatua hilyo imezusha wasiwasi wa ujumbe wao kuzuiliwa kurejea Yemen kama ilivyotokea mwaka 2016 baada ya mazungumzo ya kukwama.
Mjumbe wa maalum hajakata tamaa
Msemaji wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Martin Griffiths amesema mwanadiplomasia huyo bado alikuwa ana fanya juhudi ya kuhakikisha ujumbe wa waasi unawasili Geneva.
Kadhalika katika kipindi hicho Griffiths amekuwa na mashauriano na ujumbe wa serikali ambayo yametuama kwenye kujenga kuaminiana, ruhusa ya kupitishwa msaada wa kiutu pamoja na uwezekano wa kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege mjni Sana'a.
Yemen imetumbukia kwenye tangu mnamo machi 2015 katika vita vinashadadiwa na muungano unangozwa na Saudia Arabia ambao unaunga mkono serikali ya rais Abed Rabbo Mansour Hadi dhidi ya waasia wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.
Umoja wa Mataifa umeutaja mzozo wa Yemen kuwa mbaya kabisa wa ulimwengu ambapo baada ya miaka mitatu na nusu ya vita wayemen milioni 22 wanategemea misaada.
Mwandishi: Rashid Chilumba/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
.