1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Geneva yakamilika bila maafikiano makubwa

18 Februari 2026

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesema hatua chache zimepigwa katika mazungumzo ya mataifa hayo mawili yaliyosimamiwa na Marekani huko Geneva.

Schweiz Genf 2026 | Wladimir Medinski bei trilateralen Gesprächen zwischen Russland, USA und Ukraine
Picha: Alexander Ryumin/TASS/ZUMA/picture alliance

Rais huyo wa Ukraine amesema kando na hatua hizo, mazungumzo hayo hayakufanikiwa kufikia muafaka kuhusu suala muhimu la udhibiti wa maeneo.

Urusi inataka kuendelea kuudhibiti mji wa Mashariki mwa Ukraine wa Donetsk kama sehemu ya makubaliano yoyote yale yatakayofikiwa na imetishia kuuchukua kwa lazima iwapo Ukraine itakataa kuridhia hilo katika meza ya mazungumzo.

Ukraine imekataa sharti hilo ikisema haitotia saini makubaliano hadi pale taifa lake litakapopata hakikisho la usalama linalojumuisha Urusi kuachana na uvamizi wake Kiev. Awali Zelensky alisema anatilia shaka iwapo Urusi ina nia ya kweli ya kufikia amani huku akimuita Rais Vladimir Putin mtumwa wa vita.

Kwa upande wake ujumbe wa Urusi katika mazungumzo hayo yaliyomalizika chini ya saa mbili baada ya kuanza, ulisema majadiliano yalikuwa magumu ukisisitiza kuwa majadiliano mengine yamepangwa kufanyika katika siku za usoni.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW