Mkutano wa kimataifa dhidi ya taka za plastiki kuanza tena
22 Aprili 2024Hatua hiyo inatarajiwa miezi mitano baada ya duru ya mwisho ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Kenya.
Mwaka 2022, mataifa hayo yaliafikiana kukamilisha mwishoni mwa mwaka huu, mkataba wa kwanza wa Umoja wa Mataifa utakaoshughulikia janga la taka za plastiki zinazopatikana kila mahali huku chembechembe zikipatikana pia ndani ya damu ya binadamu na hata kwenye maziwa ya mama.
Soma pia: Mazungumzo ya kudhibiti plastiki yakumbwa na kutoelewana
Wapatanishi hao tayari wamekutana mara tatu na wanatarajiwa baada ya mazungumzo ya Ottawa, kufanya duru ya mwisho ya mazungumzo nchini Korea Kusini. Mkutano wa awali mjini Nairobi Novemba mwaka jana ulikuwa fursa ya kwanza ya kujadili rasimu ya mkataba ambao uliainisha njia za kukabiliana na tatizo hilo.