Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza kuanza tena wiki ijayo
25 Julai 2025
Kuanza tena kwa mazungumzo hayo kunajiri baada ya Israel kupitia majibu ya wanamgambo wa Hamas.
Al-Qahera imesema Ujumbe wa Israel umeondoka siku moja baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuiita nyumbani timu yake kwa mashauriano zaidi.
Hamas: Ili kusitisha mapigano Israel ijiondoe Gaza
Mshirika mkuu wa Israel, Marekani pia nayo iliwaita nyumbani wajumbe wake kwa mashauriano jana alhamisi huku mjumbe wa Marekani kwaajili ya Mashariki ya Kati Trump Steve Witkoff akiishutumu Hamas kushindwa kuchukua hatua za kufanikisha mazungumzo hayo.
Hamas imesema imeshitushwa na kauli ya Witkoff ikisema msimamo wa kundi hilo umekaribishwa na wapatanishi na umefungua milango ya kufikia makubaliano. Pande zote mbili Israel na Hamas zinapitia shinikizo kubwa la ndani na nje ya maeneo yao ya kufikia makubaliano ya kusitisha vita hivyo vinavyokaribia mwaka wake wa pili.