1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza yamalizika bila mafanikio

26 Agosti 2024

Duru ya mazungumzo ya kusaka makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza imemalizika bila mafanikio yoyote mjini Kairo, huku ujumbe wa Hamas ukikataa masharti mapya yaliyoletwa na Israel.

Watu wakikagua uharibifu baada ya shambulizi la Israeli dhidi ya shule na makazi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao, katika kitongoji cha Rimal katikati mwa Jiji la Gaza mnamo Agosti 20, 2024.
Shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: Hadi Daoud/APA Images via ZUMA Press Wire/picture alliance

Afisa huyo wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, amesema mazungumzo hayo yataendelea lakini katika ngazi ya chini siku zijazo katika juhudi za kuziba mapengo yaliyosalia.

Soma pia:Ujumbe wa Israel wawasili Cairo kwa majadiliano kuhusu Gaza

Afisa huyo amesema makundi ya ngazi za chini yatasalia mjini Cairo kukutana na wapatanishi wa Marekani, Qatar, na Misri kwa matumaini ya kushughulikia masuala ya mvutano yaliobaki.

Afisa huyo aliyatajamazungumzoya hivi karibuni yaliyoanza siku ya Alhamisi huko Cairo na kuendelea hadi jana Jumapili, kama yenye tija na kusema pande zote zilikuwa zikifanya kazi kufikia makubaliano ya mwisho na yanayoweza kutekelezwa.

Walioshiriki katika mazungumzo ya Cairo

Walioshiriki katika mazungumzo hayo ni pamoja na mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani, CIA, William Burns na mkuu wa Shirika la Ujasusi la Israel,Mossad, David Barnea.

Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah katika hotuba kupitia televisheniPicha: Hassan Ammar/AP

Ujumbe wa Hamas haukushiriki moja kwa moja katika mazungumzo hayo lakini ulipewa taarifa na wapatanishi wa Misri na Qatar.

Hezbollah yadai kulenga kituo cha kijasusi cha Jeshi la Israel

Katika hatua nyingine, kundi la Hezbollah limedai kulenga kituo cha kijasusi cha jeshi la Israeli karibu na Tel Aviv kama sehemu ya msururu wa mashambulizi ya mamia ya roketi na droni huku Israel ikidai kuwa mashambulizi yake kadhaa yalikuwa ya kuepusha shambulizi kubwa zaidi. Hakuna upande uliotoa ushahidi.

Soma pia:Hezbollah yavurumisha makombora dhidi ya Israel

Kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, amesema shambulizi hilo ambalo ni jibu la mauaji ya kamanda mmoja mkuu mjini Beirut mwezi uliopita yaliyofanywa na Israel, lilicheleweshwa kutoa nafasi kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza, na hivyo basi makundi mengine yanayoungwa mkono na Iran yanaweza kujadiliana na Iran iwapo yote yaishambulie Israel kwa wakati mmoja.

Mashirika ya vyombo vya habari yaitaka Israel kuwekewa vikwazo

Takriban mashirika 60 ya vyombo vya habari na kutetea haki za binadamu, leo yametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kusitisha makubaliano ya ushirikiano na Israel na kuiwekea vikwazo, huku yakiishtumu kwa kuwaua waandishi wa habari huko Gaza.

Wito huo umetolewa kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels tarehe 29 Agosti.