Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza yako ukingoni
15 Januari 2025Wasuluhishi kwenye mazungumzo ya kutafuta makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hamas, na kuachiliwa kwa mateka, wako katika juhudi za mwisho kufanikisha hatua hiyo, leo Jumatano.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar, Majed al Ansari amesema juhudi hizo ziko katika awamu ya mwisho na wasuluhishi wana matarajio makubaliano yatafikiwa hivi karibuni.
Soma pia: Qatar yasema mazungumzo ya usitishwaji vita Gaza yako hatua za mwisho
Taarifa zinasema jana usiku, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, alifanya mazungumzo na maafisa wake wa ngazi za juu wanaohusika na usalama kujadili mpango huo, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akisema, kinachosubiriwa ni uamuzi wa kundi la Hamas.
Blinken amefafanuwa kwamba ikiwa Hamas wataridhia mpango uliopo mezani, kitakachofuatia ni kukamilishwa na kuanza kutekelezwa.