Mazungumzo ya kuunda serikali nchini Uholanzi yakwama
27 Novemba 2023Kiongozi wa chama cha siasa kali cha Freedom kinacho chukia wageni na Waislamu na kuupinga Umoja wa Ulaya, Geert Wilders amepata pigo kubwa leo baada ya mshirika wake aliyemteua kusimamia mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto kujiondoa kwenye nafasi hiyo kufuatia tuhuma zinazomuhusisha na udanganyifu.
Hatua ya kujiondoa kwa mwanasiasa Van Strien aliyepewa jukumu la kuanza mazungumzo rasmi ya kuunda serikali baadae leo Jumatatu, imeutumbukiza mchakato huo katika mgogoro mkubwa kabla hata haujaaanza huku mikutano yote iliyokuwa imepangwa kufanyika baadae ikifutwa.
Soma pia:Chama cha siasa kali Uholanzi chajipanga kuunda serikali
Viongozi katika kanda ya Umoja wa Ulaya na kwengineko duniani wanafuatilia kwa karibu kuona ikiwa Wilders na chama chake wanaweza kuunda serikali mpya nchini Uholanzi.